-->

Roma Mkatoliki Ageukia Ualimu

Msanii wa muziki wa Hip hop, Roma Mkatoliki leo amegeukia kazi yake ya zamani ya ualimu kwa siku 1 baada ya kuamua kwenda shule ya msingi ya Mchikichini iliyopo Mbagala kuwapa hamasa wanafunzi kupenda somo la hesabu na kukabidhi vitabu vya hesabu.

Msanii Roma Mkatoliki akigawa kitabu cha hesabu kwa mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Mchikichini Mbagala

Rapa huyo anasema kuwa siku zote muziki wake umekuwa ni unaogusa maisha ya kila siku ya watu hivyo aliona anapaswa kufanya jambo ambalo litawagusa moja kwa moja na kuamua kwenda shuleni hapo kuwapa hasama wanafunzi hao kupenda somo hilo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za shule hiyo ili ziweze kutatuliwa na viongozi mbalimbali hata mashabiki wake wengine.

“Mimi kama Roma Mkatoliki, kwa kipindi kirefu toka nafanya muziki wangu zaidi ya miaka 10, muziki wangu umekuwa ukiegemea kwenye kuongelea jamii, najivunia sauti yangu inafika mbali, vitu vingi navyozungumza huwa vinafika mbali na wakati mwingine huwa vinatatuliwa baada ya kuviongea. Nikasema ngoja niguse kundi dogo, hivyo lilikuja wazo kwamba nienda Mbagala nikafika hapa Mchikichini, lengo langu lilikuwa niangalie shule iliyokuwa na changamoto nyingi zaidi ili kutoa kidogo kwa jamii. Tumekuja kuwaona darasa la saba inawezekana wazazi wao au ndugu zao ndiyo mashabiki wangu, hivyo nitatoa vitabu vya hesabu vya darasa la saba lakini baada ya hapo naamini mengi yatafuata” alisema Roma Mkatoliki

Mbali na hilo Roma Mkatoliki anasema anaamini neno lake linaweza kuwa na nguvu kubwa na kuwafanya wanafunzi hao wakapenda somo hilo na kusema anaamini wapo wasanii wengine wanaweza kuja kufanya jambo jingine kwa wanafunzi hao.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364