-->

Ruby Afungukia Tetesi za Kusaini WCB

Muimbaji wa kike mwenye sauti ya dhahabu kwenye Bongo Fleva, Ruby amefunguka juu ya tetesi zilizosambaa kuwa amesaini kujiunga na lebo ya WCB.

ruby89

Ruby

Ruby amepinga kujiunga na lebo hiyo lakini amedai kuwa anapenda kuwa karibu na Diamond kwa ajili ya kujifunza vitu vingi kutoka kwake.

“WCB hawana roho mbaya unaenda tu muda wowote kama unajua ni nini kimekupeleka pale, kwani mimi kuonekana WCB ndio nipo WCB? Diamond ni msanii mwenzangu, nikiwa naye najifunza vitu vingi, it doesn’t mean nikiwa naye nimejiunga WCB. Kumbuka pale kuna studio na kuna producer Lizer pale watu tunataka kufanya naye kazi,” amemuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Wale Wale’ aliouachia mwezi Septemba mwaka huu.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364