Sababu za Weusi Kuficha Wapenzi Wao Yafichuka
Rapa Nikki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kuweka wazi sababu ambazo zinawafanya wao kama Weusi kutoweka wazi maisha yao binafsi ikiwepo maisha ya mapenzi na maisha ya kawaida ya kila siku
Akionge kwenye kipindi cha Planet Bongo Nikki wa Pili amesema wamekuwa wakificha maisha yao binafsi kwa sababu hawahitaji familia zao au watu wao wa karibu kupata athari au madhara yanayotokana na kazi yao ya muziki.
“Unajua sisi kama wanamuziki tunafuatiliwa na watu wengi na maisha ya wanamuziki yamezungukwa na tafsiri nyigi lakini ukumbuke muziki nimetengeneza mimi kama Nikki wa Pili kwa hiyo ningependa mambo yote, madhara yote yanayoletwa na muziki yaangukie kwangu yasiende kwa mtu mwingine ambaye si kitu chake” Amesema Nikki
Ameendelea kufafanua sababu ya kutenganisha muziki na mapenzi “Kwa hiyo kama mimi nakuwa nina mtu kwenye mahusiano siwezi kumleta katika huu ulimwengu wangu ambao kwanza una mambo mengi sana ambayo yanaweza kuharibu maisha yake, ndiyo maana sisi tumeamua kutenganisha muziki siyo tu na mapenzi bali na familia hata marafiki” alisistiza Niki wa Pili
Kwa upande wake G Nako Warawara yeye alisema kuwa wao wanaishi maisha simple na ya kawaida hawakami au kutaka kuonesha kila kitu kwa jamii ili jamii ijue.
eatv.tv