-->

Ray Ashangaa Chuchu Kujifungua!

KITUKO! Wakati pongezi za kufa mtu zikielekezwa kwa muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kupata mtoto wa kiume kwa mchumba’ke, Chuchu Hans, muigizaji huyo ameibuka na kushangaa watu wanaoeneza habari za kujifungua kwa Chuchu wakati si kweli kama amejifungua.

Chuchu na Ray

Ray alitoa kioja hicho Alhamisi iliyopita wakati akizungumza na Risasi Jumamosi baada ya kupigiwa simu ili kumpongeza kwa kupata baby boy.

Awali, taarifa za uhakika zililifikia Risasi Jumamosi Jumatano iliyopita kuwa Chuchu amejifungua salama mtoto wa kiume katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar.

Baada ya kujiridhisha kutoka kwa marafiki wa karibu na kinywa cha Chuchu mwenyewe kuwa amejifungua salama mtoto huyo wa kiume, ndipo Risasi Jumamosi lilipompigia Ray bila kumueleza kwamba jana yake liliongea na mpenzi wake na mambo yalikuwa hivi:

Risasi Jumamosi: Kaka hongera kwa kupata baby boy.

Ray: Nani kasema mimi nimepata mtoto?

Risasi Jumamosi: Kaka mbona hilo lipo wazi kwamba umepata mtoto wa kiume na sisi tumejiridhisha kwa mtu wa karibu na ‘baby’ wako Chuchu.

Ray: Huyo mtu atakuwa ana matatizo, sijapata mtoto. Nifiche ya nini?

Risasi Jumamosi: Mbona unaonekana kuchenga wakati hili ni jambo la kheri?

Ray: Kaka mimi ndiyo nakuambia ukweli, najua ni jambo la kheri sasa kwa nini nifiche? Mimi nashangaa tu hii mitandao kusema nimepata mtoto sijui Chuchu kajifungua, sijui hizo habari wanazitoa wapi.

Risasi Jumamosi: Kaka kuna sababu gani ya kuficha wakati hata Chuchu mwenyewe amekiri?

Ray: Kama amesema hivyo atakuwa ana matatizo naye. Mimi sizijui hizo habari. Na huo ndiyo ukweli wangu.

Ray alikinzana na mpenzi wake Chuchu ambaye alikiri hivi alipozungumza na mwanahabari wetu siku alipojifungua:

“Daah ila namshukuru Mungu sana kwa kila jambo  na ni mwema kwangu.”

MHARIRI

Kupata mtoto ni jambo la kheri hivyo Ray hakuwa na sababu ya kuficha. Yawezekana hakujua kama mwanahabari wetu amewasiliana na mchumba’ke na kujiridhisha lakini hata hivyo hakuna kilichoharibika. Tunakupongeza Ray na tunakushauri uwe tu muwazi katika mambo haya.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364