Said Fella Afungukia Tetesi za Bifu Lake na Diamond
BAADA ya hivi karibuni kudaiwa kuwa ana bifu na msanii wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, bosi wa Yamoto Band, Said Fella amefunguka kuwa tetesi hizo siyo za kweli na haijawahi kutokea.
Habari kutoka kwa vyanzo mbalimbali zilidai kuwa wawili hao waliingia kwenye bifu baada ya wasanii wa Bendi ya Yamoto anayoisimamia kumlalamikia Diamond ambaye pia ana hisa kwenye bendi hiyo kwamba mkurugenzi wao huyo anawanyonya na kazi zote wanazopiga wao wanamnufaisha yeye tu!
Uwazi Showbiz lilipomtafuta alisema: “Hakuna kitu kama hicho na haijawahi kutokea kabisa, hayo ni maneno tu ya watu na wala mimi na Diamond hatujawahi kuzungumza kitu kama hicho.”
Chanzo:GPL