-->

Salome ya Diamond Ilivyobadili mipango ya Darassa Kwenye Wimbo ‘Muziki’

Hit maker wa wimbo Muziki, Darassa amedai hapo awali alikuwa ana mpango wa kumshirikisha Saida Karoli kwenye wimbo wake ‘Muziki’ lakini baada kuona Diamond ametoa wimbo ‘Salome’ ambao ndani yake amemtumia Saida Karoli akaamua kuusitisha mpango huo.

Rapa huyo amedai wazo la kumtaka kumshirikisha muimbaji huyo wa muziki wa asili wa zamani lilitokana na mdundo wa wimbo huo.

“Wakati tumemaliza kutengeneza mtu akatushauri kwanini msimtafute Saida Karoli kwa sababu huu mdundo una mahadhi ya Kiafrika na Saida Karoli alikuwa anaimba mahadhi ya Kiafrika, kwanini msimtafute mkamuweka ili muimalize hili idea. Kwa sababu mtakuwa mmemchanganya msanii wa kisasa na wazamani nikaona sawa ni wazo zuri,” Darassa aliimbia Global TV. “Lakini kabla ya kuzungumza na Saida Karoli na kumsikilizisha wimbo pamoja na kumpatia wazo tayari ukawa umeshatoka wimbo wa Salome wa Diamond akiwa na Rayvanny so tukaona hakuna haja tena ya kuendelea na hii project,”

Kwa sasa rapa huyo anafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga kupitia wimbo wake, Muziki ambao umependwa zaidi na mashabiki katika kipindi cha muda mfupi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364