Sauti ya Mama Wema Ingenitoa Roho – Steve Nyerere
MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefunguka kuwa, kama si ujasiri wa kiume, sauti iliyovujishwa na mama wa mwigizaji Wema Sepetu, Miriam, akisikika akiwataja baadhi ya viongozi kushirikiana naye ili kumsaidia Wema atoke sero, ingemsababishia kifo kwa presha.
Nyerere alisema suala hilo limshtua kiasi ambacho aliona dunia yote itamlaumu yeye hivyo anamshukuru Mungu alisimama kama mwanaume na kufafanua ukweli wa jambo lenyewe.
“Unajua yale yalikuwa mazungumzo ya kumtoa njiani mama Wema, nikawaweka hadi waheshimiwa mawaziri mle ndani ili tu kumpoza yule mama asijisikie vibaya na kuona mwanaye tumemtenga lakini niliposikia yamevuja, nilipata shida sana kuona waheshimiwa watanielewaje?” alisema Steve.
Hata hivyo, Steve alisema alishamsamehe mama Wema kwa kuvujisha video hiyo na sasa anaendelea na maisha yake kama kawaida kwani suala hilo limepita.
Chanzo:GPL