Shamsa Ford Amkana Nay wa Mitego
Malkia wa filamu Shamsa Ford amekanusha kuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’ ya rapa Nay wa Mitego itayofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, May 20 mwaka huu.
Muigizaji Shamsa Ford Rapa huyo hivi karibuni aliimbia Bongo5 kuwa muigizaji huyo ambaye kwa sasa ameolewa na mfanyabiashara Chidi Mapenzi, atakuwepo kwenye show hiyo.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Shamsa amedai hajui chochote kuhusu show hiyo.
“Kusema kweli sina show yoyote na mtu na wala sijazungumza na Nay wa Mitego kuhusu show ya Dar Live,” alisema Shamsa Ford.
Aliongeza,”Hajaniambia chochote siwezi kudanganya, ndio kwanza hizo taarifa naziona katika mitandao ya kijamii. Kama kweli na mimi nitakuwepo ungeona hata nikipost. Kwahiyo sitakuwepo kwenye hiyo show kwa sababu sina taarifa yoyote,”
Wiki iliyopita rapa Nay wa Mitego alidai licha ya kuachana na muigizaji huyo na kuolewa na mtu mwingine lakini wanashirikiana katika mambo mbalimbali.
“Wapo Tour itakuwa ni ya Kipekee sana kwani itakuwa na list ya wasanii wawili watatu hivi wa kunisindikiza, lakini pia atakuwepo Shamsa Ford kwenye special appearance pia atakuwa kama MC kwa siku hiyo jukwaani,watu watarajie kuona burudani ya kipekee kabisa,” alisema Nay wa Mitego.
Bongo5