-->

Shamsa Ford Apata Majanga, Apigwa Ngumi

STAA wa kutoka kiwanda cha filamu cha Bongo Muvi, Shamsa Ford amepata jeraha la maisha baada ya kupigwa ngumi na jamaa ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shamsa alitupia picha iliyomuonyesha akiwa na jeraha usoni na kuandika ujumbe kwa mashabiki zake kuwa alipigwa akiwa anagombelezea ugomvi.

Shamsa amefunguka kuwa tukio limetokea wakati alipoingilia ugomvi kwa lengo kuamua jamaa anayedaiwa kuwa ni mpita njia.

Inadaiwa jamaa huyo alikuwa akimtongoza hausigeli wa Shamsa kwa kumshikashika sehemu za mwili wake kwa nguvu. Hapo ndipo Shamsa aliingilia kati na kupigwa kibao baadaye ngumi ya uso.

Kwa sasa Shamsa anaendelea vizuri japo alikuwa akilalamika maumivu makali kichwani.

Chanzo;GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364