Shamsa Ford Awatia Moyo ‘Single Mothers’
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford ambaye ameolewa siku za karibuni amewatia nguvu wanawake ambao wanalea watoto peke yao bila wazazi wa kiume.
Shamsa amesema kuwa licha ya yeye kuolewa sasa lakini bado ataendelea kuwa pamoja na wanawake wale ambao wamekuwa wakilea watoto Wao wenyewe bila kushirikiana na wanaume.
Shamsa Ford anasema kuwa wanawake hao wanapitia matatizo mengi hivyo ni vyema waendelee kusaidiana kimawazo na kwenye matatizo ikiwa ni pamoja na kutiana moyo kwa changamoto mbalimbali wanazopitia.
“Pamoja na kwamba nimeolewa lakini bado nipo bega kwa bega na all ‘Single Mother’s’ nikimaanisha wanawake ambao wanalea watoto wao wenyewe bila msaada wa mzazi mwenzie. Nilikuwa huko najua tunayoyapitia ni matatizo ambayo tunakutana nayo. Nitaendelea kuwapa moyo na mawazo mbalimbali. Inshaaallah natamani kabla huu mwaka haujaisha nikutane na ‘all single mother’s’ ili tuweze kutiana moyo na kujua jinsi ya kusaidiana” alisema Shamsa Ford
eatv.tv