Shilole Ataja Tarehe ya Ndoa Yake
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amesema mipango ya ndoa yake sasa imeiva, anatarajia kufunga Oktoba, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Shilole alisema maandalizi yanaendelea na sasa zoezi lililobaki ni kutoa kadi za mwaliko kwa ndugu, jamaa na marafiki.
“Mipango ya ndoa inakwenda vizuri, hivyo Oktoba mwaka huu utakuwa mwezi wetu ambao Mwenyezi Mungu atatubariki kuunganisha familia,” alisema Shilole.
Shilole alisema kwa hatua hiyo aliyofikia, anamshukuru Mungu na amewataka wasanii wenzake na mashabiki kumpa sapoti katika ndoa yake.
Mtanzania