Shilole Afunguka Kuhusu Kupigana Na Mumewe Uchebe.
Msanii wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema hawezi kuthubutu kwa sasa kupigana na mume wake Uchebe kwani sasa amekuwa mtu mzima na mapenzi ya kupigana yalikuwa ya utoto. Shilole amebainisha hayo kupitia eNewz inayorushwa na EATV baada ya kuzoeleka na watu wengi kwa tabia yake ya kupiga wanaume ambao anakuwa nao
Amefunguka na kusema kuwa hakupigana na mume wake Uchebe kama taarifa zinavyosambazwa katika mitandao ya kijamii.