-->

Shilole Afuta Tattoo ya Nuh Kifuani, Yasemekana Penzi Lao Limeingia Mchanga!

Kuna taarifa mtaani kuwa penzi la mastaa wa muziki, Shilole na Nuh Mziwanda limevunjika. Japokuwa sio mara ya kwanza kwa tetesi kama hizo kuhusu couple hiyo, lakini safari hii kuna dalili kuwa inaweza kuwa ‘serious’.

shilole-2

Moja ya vitu vinavyoongeza nguvu ya tetesi hizo, Shishi amefuta ile tattoo aliyochora kifuani kwake miezi kadhaa iliyopita, yenye jina la ‘Nuh’ na kuchora UA juu yake.

SHISHI tattoo mpya
Tattoo mpya

shishiiiii

SHISHI tattoo zamani
Tattoo iliyofutwa

Kipindi cha karibuni wawili hao hawaonekani pamoja kama ilivyozoeleka, na kila mmoja amefuta picha zao za pamoja kwenye akaunti zao za Instagram. Pia weekend iliyopita Shishi alifanya sherehe nyumbani kwake ambayo hakusema sababu ya sherehe hiyo, lakini hakuwa na Nuh na wala hakupenda kumzungumzia pale alipoulizwa na marafiki aliowaalika.

Chanzo:  Bongo5.com

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364