-->

Shilole Atoboa Siri ya Kuolewa Kimya Kimya

Msanii Zuwena Mohamed, maarufu kama Shilole amesema kilichomfanya afunge ndoa kimya kimya ni kutokana na ushauri alioupata  kutoka kwa Maustadhi kuwa siku ya ndoa ina mambo mengi na ‘husda’ nyingi, ndio maana alifunga ndoa kimya kimya.

Shilole alitoa ahadi kuwa atafunga ndoa  kabla ya mwaka huu kuisha na kuwahaidi  mashabiki wake kuwa atawatangazia siku ya ndoa yake lakini hakutekeleza ahadi yake hiyo na badala yake mashabiki wake waliona tu picha zake akiwa  tayari amefunga  ndoa.

“Mimi tayari nimeshafunga ndoa kama mlivyoona picha lakini naomba mashabiki zangu msijali ndoa tayari lakini kutakuwa na sherehe kati ya tarehe 20 au 25 mwaka huu kwahiyo mashabiki wangu mjiandae kula na kusaza mpaka vyakula vingine mtaondoka navyo,”amesema Shilole

Siku chache zilizopita  Shilole alifunga ndoa na mpenzi wake Uchebe na kesho yake picha kusambaa mitandaoni

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364