Shilole Awafungukia Wanaomuhusisha na Nuh Mziwanda
Msanii wa bongo fleva nchini Tanzania Shilole ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ”Hatutoi kiki’ amewataka watu kuacha tabia ya kuendelea kumzushia vitu ambavyo sio vya kweli baina yake na Nuh Mziwanda.
Hayo yamekuja baada ya kuzagaa kwa picha zinazowaonesha wakiwa pamoja katika mapozi ya kimapenzi jambo ambalo Shishi amesema siyo la kweli ila watu ndiyo wanavumisha hivyo vitu.
“Mimi na Nuh ni washikaji tu, halafu Mwanza hatujakatana katika ‘show’ ila kila mtu alikuwa kwenye mishe zake hivyo sijaona tatizo la mimi kusalimiana naye pamoja na kupiga picha kwa kuwa alikuwa ‘Ex boyfriend’ wangu na nimeishia naye takribani miaka 5 watu waache tabia ya kukuza vitu ambavyo hawana uhakika navyo”. Alisema Shilole kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio
Aidha Shilole amesema anampenda Barnaba kwa kuwa ndiyo mtu pekee anayemsaidia katika kuandika mashairi ya wimbo ambazo anazitoa hata ‘Hatutoi kiki’ ameandika msanii huyo.
Kwa upande mwingine Shishi baby amewataja wasanii wake watano anaowakubali kila wakati kusikiliza ngoma zao wakiongozwa na malkia wa taarabu Khadija Kopa, Mwasiti, Linah, Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny.
eatv.tv