-->

Snura: Natamani Nimrudie Mungu

MSANII aliyetamba na wimbo wa Chura, Snura Mushi, amesema malengo yake makubwa ni kumrejea Mungu kabla hajaaga dunia.

Snura alisema imani yake ni kwamba mambo ya dunia yana mwisho wake, hivyo kuamua kuwa mlezi wa madrasa aliyoachiwa na marehemu babu yake iliyopo Yombo Vituka, kama njia ya kumrudia Mungu.

“Najitahidi kufanya kazi kwa bidii na maombi yangu kwa Mungu ni aniwezeshe niweze kumtumikia kabla siku yangu ya kufa maana natamani ifike siku niachane na masuala ya kidunia, nijielekeze kwenye dini,” alieleza Snura.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364