Shilole Awajibu Wanaoiponda Ndoa Yake
MSANII wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amefunguka na kusema wanaoiponda ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii wana chuki binafsi.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Shilole alisema tangu afunge ndoa na mpenzi wake Uchebe, kumezagaa maneno ya majungu kitu ambacho hakiwezi kumkatisha tamaa na anaamini ndoa yake itadumu.
“Mfa maji aishi kutapatapa, ndoa yangu imewaumiza wengi wasionipenda, nimeona maneno ya kashfa na majungu wakinichafua, sasa mimi nasonga mbele na maisha yangu sina habari na mtu,” alisema Shilole.
Aliongeza kuwa familia yake imelipokea jambo hilo vizuri, licha ya kutokea migogoro ya hapa na pale lakini ni mambo ya kifamilia na wameyamaliza.
Mtanzania