-->

Shilole na Uchebe wafunguka kuhusu ndoa kuvunjika

Msanii wa muziki bongo ambaye kwa sasa mjasiriamali anayehakikisha matumbo ya watu yanapata afya, Shilole au Shishi Trump, hatimaye amefunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na mume wake Uchebe.

Akizungumza na mwandishi wa EATV Shilole amesema hajaachana na mume wake na wala hawafikirii kuachana.

Kwa upande wa mume wake Shilole Bwana Uchebe amesema sio kweli kwamba ameachana na mkewe, na kwamba kuna wanafiki wanapenda wasikie wameachana.

Akifunguka kuhusu kupost kwa ua jeusi na caption yenye utata, Uchebe amesema kuna mtu alihack acount yake na kupost hivyo, lakini hawajaachana namkewe na wala sio kiki.

“Sio kweli sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi, na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”, amesema Uchebe.

Tetesi za wawili hao kuachana zimekuja baada ya kupostiwa kwa ua jeusi kwenye ukurasa wa instagram wa Uchebe na caption ambayo ilikuwa na utata, na watu kuhisi labda wawili hao hawako pamoja tena.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364