-->

Shilole: Watoto Wangu Hawataiga Maisha Yangu

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amesema kwamba watoto wake hawataiga maisha wala mavazi anayovaa kwenye shoo zake wala maisha ya sanaa anayoishi kwa kuwa wanatambua yupo kazini kwa ajili yao.

Shilole akiwa na mtoto wake

Shilole aliliambia MTANZANIA kwamba, malezi anayowalea watoto wake ni tofauti na maisha anayoishi yeye na watoto hao wanatambua kwamba mama yao ni msanii hivyo hawataiga anachofanya.

“Watoto wangu nawalea katika maadili kama mama, siwezi kuwalea maisha ya kistaa kama ninavyoishi mimi na wanatambua kwamba mama yao nipo kazini kwa ajili yao na pia hawana ndoto za kuishi maisha yangu ya kisanii,” alieleza Shilole.

Shilole aliongeza kwamba licha ya kulea watoto wake kwa maadili ya dini, lakini hataacha kuendelea kuwapa elimu, mafunzo ya maisha na biashara.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364