Chuchu Nanyonyesha na Bado Nafunga
MSANII wa filamu Bongo Chuchu Hans amesema licha ya kumnyonyesha mtoto wake aitwaye Jaden, bado ataendelea kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwani kama ni wingi wa maziwa, atahakikisha anakula vizuri baada ya kufuturu.
Akipiga stori na Za Motomoto News, alisema yeye ni Muislam anayezingatia maadili ya mfungo, hivyo kitendo cha kuwa na mtoto mdogo ambaye ana umri wa miezi minne hakiwezi kumzuia kuacha kufunga, anachohakikisha ni kumpa mlo kamili na yeye kupata shibe stahiki.
“Muda wa kufunga nahakikisha anakula chakula cha kutosha ili asijisikie vibaya kukosa maziwa ya mama, lakini nikishafungua najitahidi kula vizuri ili maziwa yasitoke kwa shida, mwanangu anyonye ipasavyo, huu ni mwezi wa pekee, sitaki unipite bila kuuzingatia matakwa yake,” alisema Chuchu Hans.
Chanzo:GPL