-->

Shirikisho la Filamu Lazipokea ‘EATV AWARDS’ kwa Mikono Miwili

Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) limezipokea EATV AWARDS kwa mikono miwili na kutoa baraka zake, huku wakisema ni jambo jema kwa tasnia ya filamu kwa sasa, ukizingatia tasnia hiyo kwa sasa inapigana iweze kwenda mbele zaidi.

Simon Mwakifwamba

Simon Mwakifwamba

Akizungumza na mwandishi wa EATV Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, amesema tuzo hizo zitasaidia kuleta changamoto kwenye tasnia, na ushindani utakaoleta uhai wa filamu za Tanzania na wasanii wake.

“Tumezipokea vizuri kwa sababu uwepo wa tuzo kunaleta ushindani, kunaweka uhai kwa tasnia ya filamu, kuwepo kwa tuzo ni fursa kwa waandaaji ni fursa kwa waigizaji, madirector na producers, kwa hiyo sisi tunasema tuzo ni jambo zuri, ni jambo la msingi na tuna-suport, kikubwa ni kuhamasisha watu waweze kujitokeza, kwa sababu watu watakavyojitokeza kwa wingi ndio ushindani unapokuwa mkubwa zaidi kuliko wakijitokeza watu wachache, ushindani nao unakuwa mdogo’, alisema Mwakifwamba

Bw. Mwakifamba aliendelea kwa kuishauri EATV ambao ndio waandaaji wa tuzo hizo, kutenda haki wakati wa ugawaji wa tuzo hizo, ili kuepuka migogoro kwa wahusika pamoja na kuzingatia vigezo katika kutafuta washindi wa tuzo.

“Kitu kingine haki itendeke haswa kwa upande wa majaji katika kuamua, kwa sababu kunakuwaga na changamoto kwenye vitu hivi, unakuta mtu anapewa tuzo huyu analalamika huyu hakustahili, huwezi kuwaridhisha watu wote lakini iwe ‘serious’ ionekane, kwamba hawa jamaa majaji walitumia vigezo, weledi, kwa hiyo ni suala la kuliangalia”, alisema Mwakifamba.

Bwana Mwakifamba alimaliza kwa kuwataka wasanii kujitokeza kushiriki kwenye tuzo hizo, ili waweze kuweka rekodi nzuri kwenye kazi zao, kwani ni moja ya vigezo vitakavyowawezesha kupata fursa kubwa zaidi.

“Wasanii wajitokeze kwa sababu leo kama movie yako imeshinda, tayari umejiwekea kwenye rekodi, na rekodi hauwezi ukawa nayo kama umekaa nyumbani, lazima ujitokeze, uingie kwenye ushindani, na ukishinda basi watu waseme fulani bwana ndiye mshindi, wasibweteke tu kukaa nyumbani, au kuona tu kazi zangu mimi nisha-release watu wananifahamu, hiyo peke yake haitoshi, kwa sababu katika kazi tunahitaji kuona CV”, alisema Mwakifamba.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364