-->

Sholo Mwamba: Man Fongo Kabweteka Mapema Sana!

MKALI wa Muziki wa Singeli ambaye alisikika katika Ngoma ya Kazi Kazi ya Prof. Jay, Sholo Mwamba kwa mara ya kwanza amemfungukia msanii mwenzake, Man Fongo kuwa kwa muda mfupi aliotoa ngoma ya Hainaga Ushemeji imemfanya kubweteka na kuridhika.

shoro-5-001

holo Mwamba

Akichonga mbili-tatu na Global TV Online kupitia Kipindi cha Mtu Kati, Sholo Mwamba anayetikisha na Ngoma ya Sembe Tembele alisema, Man Fongo alikuwa DJ wake na hata mwanzoni alikuwa akitumia jina la Man Fongo Mwamba.

“Zamani Man Fongo alikuwa DJ wangu, kipindi napata shoo za mkoa nilikuwa nikimuachia kitengo ambapo kama sipo walikuwa wakimuita Man Fongo Mwamba. Ukaribu ukaenda sana, nimekuwa naye kwenye maisha magumu yote tatizo lake alipotoa ngoma ya Hainaga Ushemeji anaona tayari kamaliza kila kitu wakati safari bado ndefu.

“Ukisikiliza hapa kati baada ya Hainaga Ushemeji ametoka wimbo wa Kibaka na mwingine lakini zote bado hazijafikia ubora wa Hainaga ushemeji hapo utaona kwa jinsi gani alivyobweteka kuishi na ngoma moja na kushindwa kufanya ngoma kali kuzidi ya kwanza,” alisema Sholo Mwamba.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364