Sijakimbia Jiji Nimeokoa Kipaji Changu- Luckey
LUCKEY LUCKAMO mwigizaji wa kiume kutoka Bongo Movie amefunguka kwa kusema kuwa aliamua kurudi kwao Tanga baada ya kubaini kuwa ukihamia Dar es Salaam kama mwigizaji mzuri unapoteza uhalisia kwa sababu kuna aina moja ya uigizaji hivyo ushindani unapotea ghafla baada ya kugundua hilo kwa sababu yeye ana malengo makubwa aliamua kurudi zake sehemu ambayo anaamini ndio chimbuko la filamu Bongo.
“Ukiisoma tasnia kwa umakini unaepuka kupotea nilisoma game kwa muda na kubaini mambo ambayo haikuwa rahisi kuyaona kama haujui sanaa, nikagundua kuwa vijana kama mimi tunaigana kwa sababu tupo pamoja nikaamua kurudisha mpira kwa kipa,”alisema Luckey
Msanii huyo ambaye pia ni muongozaji na mtunzi wa filamu Bongo amesema kuwa amejikita jijini Tanga akiandaa sinema zake ambazo zimelenge kuelimisha jamii na si kula bata tu kila siku kama ilivyozoeleka katika sinema zetu na anataka kuonyesha jamii kuwa filamu chimbuko lake Tanga ilipoanzia Shamba kubwa Dunia Hadaa na filamu kama Love story Tanganyika na Unguja.
Filamu Central