-->

Sijawahi Kulala kwa Shilole – Nedy Music

Msanii wa bongo fleva kutoka PKP chini ya Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kuwa na mahusiano na msanii mwenzake Shilole, na kusema kuwa hajawahi kuwa mahusiano na mwana dada huyo zaidi ya urafiki wa kawaida.

Nedy Music akiwa na Shilole

Nedy akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV alisema taarifa za kuwa yeye ni miongoni mwa vijana waliotongozwa na Shilole siyo za kweli na kwamba hajawahi kulala kwa Shilole kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

Shilole amkuwa kwenye mahisiano na wasanii kadhaa akiwemo Hamadai na Nuh Mziwanda ambao tayari ameachana nao na hivi karibuni ukaribu wake na Nedy Music umeibua maswali na hisia miongoni mwa mashabiki kuwa huenda wawili hao wapo kwenye mahusiano.

Katika hatua nyingine, Nedy alisema kuwa kuondoka kwa Mubenga kwenye lebo yao ya PKP hakujaacha pengo lolote kwa kuwa menejimenti bado ipo licha ya kutokakuwa na meneja.

“Kuondoka kwa Mubenga hakujaacha pengo lolote lakini mpaka sasa hakuna aliyeziba nafasi yake, mambo yanakwenda vizuri na muda ukifika tutamuweka wazi meneja mpya” Alisema Nedy ambaye alikuwa akitambulisha ngoma yake aliyoshirikiana na Christian Bella.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364