-->

Gabo: Mtindo wa Maisha Yangu ni Tofauti na Wenzangu

Msanii Gabo Zigamba ameweka wazi kuwa hana tofauti na wasanii wenzake kama ambavyo imekuwa ikilalamikiwa na wengi kuwa msanii huyo haelewani na wenzake.

Gabo Zigamba

Akizungumza na East Africa Television, Gabo amesema kinachomfanya aonekane ana tofauti na wasanii wenzake ni utoafuti wa mtindo wa maisha alionao, lakini hana tatizo nao na anawapenda kwa dhati.

“Hakuna msanii ambaye sielewani naye, sema lifestyle yangu mimi ndiyo haifanani na wao, lakini naelewana na wasanii wote nawapenda wananipenda, mimi nawapenda kwa dhati ya moyo, sijui wao kama wananipenda kwa nafsi ya uso, ila sina kikwaruzo, sina ugomvi, ila utofauti unapoonekana unaweza mtu ukakunja kwa sababu ndiyo tatizo la watanzania, ila mimi niko sawa nao labda wao wasiwe sawa na mimi”, alisema Gabo.

Gabo aliendelea kusema kwamba tofauti kubwa iliyopo kwake na wasanii wenzake ni matarajio yake ya kufanya utofauti kwenye tasnia ya filamu hapa nchini.

“Unajua kila mmoja ana nafasi yake kwa mashabiki wake, siwezi nikasema najiona tofauti na wao, ila naweza kusema natarajia kufanya vitu tofauti na wao walivyovifanya”, alisema Gabo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364