-->

Sijawahi Kuomba Kolabo kwa Msanii wa Bongo – Q Chief

Msanii nguli wa bongo fleva Q Chief amesema hajawahi kumpigia msanii yoyote hapa Tanzania kumuomba wafanye kolabo japo yeye amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali wakimuomba kufanya naye kolabo.

qchief

Akiongea ndani ya eNewz Q Chilla amesema huwa anaangalia muda wake pale anapopigiwa simu za kuombwa kolabo na  mara nyingi anaangalia malipo na muda aliamua kuchukua maoni ya watu walipomshauri kuwa akitaka kupiga kolabo afanye na Diamond kwa kipindi hiki ndiyo akaamua kuufanyia kazi ushauri wa mashabiki zake.

Pia Q Chilla hakusita kumsifia King Kiba kuwa anastahili kuwa KING na anapenda ngoma zake ila kuna utofauti kati yao hivyo watakapo kutana kwenye kolabo ni lazima wafanye wimbo wa tofauti sana kwa kuwa wote ni wakali wa voko.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364