-->

Sijawahi Kupata Tuzo Tangu Nianze Muziki -Mr. Blue

Msanii wa Bongo Fleva nchini Mr. Blue ameweka bayana kwamba pamoj na kukubalika na mashabiki wengi na na kuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu hajawahi kupata tuzo hata moja ya kutambua mchango wake kwenye muziki.

mr-blue

Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa, Mr. Blue amesema  anatambua umuhimu wa msanii kupata tuzo ila kwa bahati mbaya yeye hajawahi kupata tuzo.

“Mimi sijawahi kupata tuzo yoyote siyo ya kitaifa wala ya kimataifa ila ninachoamini mimi ni kwamba mimi ni ‘expensive’ na ndiyo maana natoa ngoma mara moja kwa mwaka na inadumu kwa muda mrefu” Amesema Mr. Blue

Aidha Mr. Blue ameongeza kuwa tuzo ambazo zimeanzishwa na EATV zitasaidia sana wasanii wengi kuweza kutambulika zaidi na anaamini pengine anaweza kupata tuzo hiyo na ikawa tuzo yake ya mara ya kwanza.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364