Hii Ndilo Jina Jipya la Mr Blue Baada ya ‘Simba’ Kupokonywa
Mr Blue amelitaja jina lake jipya analolitumia baada ya lile la ‘Simba’ kuchukuliwa na Diamond Platnumz.
Rapper huyo amesema kuwa kwa sasa anatumia jina la ‘Nyani Mzee’ kama jina lake jingine la utani.
“Actually kwa sasa jina la Simba nimeliacha ila kwa sasa natumia jina la ‘Nyani Mzee’ nikimaanisha nimekwepa mshale mingi. Nasubiri na hilo wachukuwe nitafute jina jingine,” amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mwezi Disemba mwaka jana Mr Blue na Diamond waliingia kwenye mzozo kuhusiana na jina la ‘Simba’ huku kila mmoja akidai ni lake.
Bongo5