-->

Sikumfukuza Young D – Max Rioba

Aliyekuwa mlezi na meneja wa Rapa Young D, Maximilian Rioba amefunguka na kuweka sawa kuwa yeye hakumfukuza Rapa huyo nyumbani kwake bali alimwambia tu aondoke kwani walishindwana kibiashara kutokana na utovu wa nidhamu.

Young D na Maximilian Rioba

Maximilian akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live alisema sababu kubwa iliyompekelea kushindwana kibiashara na Young D ni kutokana na msanii huyo kutokuwa na nidhamu ikiwa pamoja na kukiuka utaratibu wa kazi.

“Mimi sikumfukuza Young D bali nilimuomba aondoke na aniache niwe huru maana unajua kumfukuza mtu ni tofauti na kumuomba aondoke hivyo sikumtolea vitu nje na kusema ondoka bali nilimweleza tu anipishe na akafanya hivyo. Utovu wa nidhamu ni moja sababu mimi na Young D kushindwana kibiashara haiwezekani msanii wangu anafanya show mimi naona kwenye Instagram nakuuliza unasema oohh tulipanga kukueleza, unafanya hivyo mara ya kwanza mara ya pili na mara ya tatu” alisema Max Rioba

Mbali na hilo Max anadai yeye hana kinyongo na Yound D kwa kuwa anamuheshimu sana ila anamuombea Rapa huyo aweze kujitambua kwani bado ananafasi kubwa ya kufanya vyema katika muziki, bado ananafasi kubwa ila anapaswa kujitambua saizi kwa kuwa yeye ni baba sasa.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364