-->

Sina Mpango wa Kubadili Jina – Harmo Rapa

Msanii wa bongo flava ambaye ndiyo anaanza kuchipukia, Harmo Rapa, amesema kuwa hana mpango na wala hawezi kubadili jina hilo lililompa umaarufu kwenye muziki kwa hofu ya kupoteza mashabiki wake.

Harmo Rapa

Msanii huyo anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘USIGAWE PASI’. ametoa msimamo huo kupitia eNewz ya EATV iliyomtafuta kuzungumza naye kuhusu mpango wa kubadili jina lake na kutotumia jina la ‘Harmo Rapa’.

“Mimi sina mpango wa kubadili jina langu kwa sababu naogopa kupoteza mashabiki zangu na ukiangalia kwa sasa jina la Harmo Rapa limeshakuwa kubwa na tayari nimeshajitengenezea mashabiki kupitia jina hilo”

Pia amesema kuwa hana mpango wa kwenda WCB na wala hahitaji msaada wowote kutoka kwao huku akionesha jeuri kuwa angeweza kutoka hata bila kutumia jina hilo. “Hata bila kufananishwa na Harmonize mimi ningetoka tu”

Harmo Rapa ni moja kati ya wasanii ambao wamepata kiki ya kutosha kutokana tu na muonekano wake ambapo watu wengi wamekuwa wakimfananisha na Harmonize kutoka WCB.

Msanii huyo hivi karibuni katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alijifananisha na Fid Q na kuwaacha watu midomo wazi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364