-->

Video: Vita ya Maneno kati AY na Mona Gangstar Yafikia Patamu

Msani wa bongo fleva AY amewataka watayarishaji wa muziki kuwa karibu na wasanii wao kila wanapoenda kwenye ‘tour’ mbalimbali ili kuweza kujifunza mambo mengi zaidi na kuongeza ubunifu.

Akiongea kupitia eNewz AY amesema alipotoa hiyo kauli aliitoa kama wazo lakini producer  Mona Gangstar amesema yeye anawaza pesa na siyo kuzurura na msanii ili kuongeza ufahamu wake kwa kuwa wasanii hawapendi kulipa hela nzuri studio.

Hata hivyo Mona amemsihi AY kuwashauri wasanii wenzake  kulipa vizuri studio  na AY pia amemsihi Mon kuacha kufanya kazi na wasanii ambao hawapo tayari kumlipa pesa producer pale anapofanya kazi nzuri.

Tazama hapa video kama walivyowekwa kati kwenye eNewz

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364