-->

Sina Urafiki na Bongo Movie Zaidi ya Kazi- Gabo

MUIGIZAJI bora katika tasnia ya filamu Bongo Salim Ahmed ‘Gabo’ amesema kuwa hana rafiki ndani ya Bongo movie zaidi ya kazi kitu anachokipenda kuliko kitu kingine , alisema kuwa anakuwa na rafiki katika kazi husika tu na si vinginevyo hivyo anashanga kutokea mtu kumshambulia katika mitandao ya kijamii.

 

“Niwe wazi kiukweli naweza sina rafiki Bongo movie mimi napenda kufanya kazi na kuondoka kam animemaliza kazi sina sababu ya kuzubaa sehemu hiyo naendelea na kazi zangu sijawahi kumletea dharau msanii mwezangu,”alisema Gabo.

Siku za karibuni msanii Duma aliibuka na kumshutumu Gabo kwa matukio mbalimbali akidai kuwa hawaheshimu wasanii wakubwa walioanza kuigiza kabla yake, pamoja na masuala kuchukua nafasi kubwa katika mitandao hakujibu huku akisema kuwa jibu la mwelevu ni kuwa na subira na sikujibu kila tukio bila kupima.

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364