-->

Sipendi Watu Wanaotembelea Nyota za Watu- Esha Buheti

ESHE Buheti mwigizaji bora wa kike wa filamu Swahilihood amefunguka kwa kusema kuwa kuna baadhi ya watu upenda kutembelea nyota za wengine kwa kujitengenezea sifa bila kuwatambulisha wale waliofanya kazi hiyo bila kujua kuwa kufanya hivyo ni wizi au uharibifu kwa mhusika aliyetengeneza kitu hicho.

Esha Buheti

Esha Buheti

“Kuna watu wanakera sana katika dunia hii unakuta mtu umetengeneza kitu chako kizuri halafu mtu anakichukua na kuwa wa kwanza kukiposti Instagrama na kujinadi kama ni yeye aliyetengeneza au ndio mpishi tunaharibiana,”anasema Eshe.

Mwanadada huyo anasema kuwa kama mtu anataka kutumia picha za msanii ambazo pengine zinamtangazia biashara ni bora kumjulisha au kuwa wazi kwa kusema ukweli kuwa kazi hiyo imefanywa na nani na si kujisifia kuwa mtu anayeposti kuwa ndio kazi yake hiyo ni sawa na kupora haki ya mtu na kumharibia biashara yake kwa wateja wake.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364