-->

Sitamtambulisha Mpenzi Wangu Tena – Nisha

Msanii machachari wa bongo movie Nisha Bebe amesema hatorudia kosa la kumtambulisha mpenzi wake kwa sasa bali atamtambulisha mume wake akiwa tayari.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Nisha amesema  “Sirudii makosa kwa sasa hivi wasitarajie kumsikia mpenzi wangu wala kumtambulisha kwa jamii mtu nitakaye kuja kumtambulisha ni mume wangu ambaye tayari nishampata ila tunachunguzana tabia kwanza kwa sasa” aliongea Nisha

Hata hivyo Nisha aliendelea kusema kwamba hata kama itamchukua muda mrefu kujuana tabia na mume wake mtarajiwa haijalishi ili mradi waweze kujuana vizuri na

“Watu wasitarajie kuona dalili yeyote ya kumtambulisha mpenzi wangu kabla hatujaoana”Alimalizia Nisha.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364