Sitegemei Muziki Kuishi Mjini – Shetta
Rapa anayewakilisha Ilala, Shetta ‘Baba Qayllah amefunguka na kudai kwamba haishi kwa kutegemea kufanya ‘show’ ndio maana maisha yake hajawai kuyumba hata kama asipotoa nyimbo kwa muda mrefu.
Shetta amefunguka na kusema hizo hizo pesa anazokusanya kwenye muziki amewekeza kwenye biashara kubwa na ndogo ambazo zinamkimu yeye pamoja na familia yake na siyo ‘show’ za muziki ambazo zinamuweka mjini kiwani wakati mwingine huwa anazikataa kwa kuwa hayajafikia masharti ya mahitaji yake.
“Wasanii wengi maisha yao yanayumba kwa sababu wanategemea show. Mimi nimewekeza kwenye biashara ndogo ndogo ingawa ambao hawajui wananituhumu kwa kujishughulisha na biashara haramu. Kwa hiyo usijiulize sana napata wapi pesa za kuishi maisha mazuri au kubadilisha magari. Project kibao zipo matangazo pia nalipwa siyo muziki tu” Shetta alifunguka.
Shetta ameongeza kwamba mara nyingi amekuwa anakataa kufanya show zinazomlipa hela kidogo ili kuendelea kukuza jina na ‘brand’ yake.
eatv.tv