-->

Sitochora Tena Tattoo ya Jina la Mpenzi Wangu – Shilole

Shilole ameapa kutorudia tena kuchora tattoo yenye jina la mpenzi wake.

SHISHI-tattoo-mpya

Hivi karibuni muimbaji huyo alilazimika kuifuta tattoo ya jina la aliyekuwa mpenzi wake, Nuh Mziwanda.

Shilole amesema kujichora tattoo ya jila Nuh kumemharibia issue kibao.

“Tattoo hapa ni empty,” aliambia 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii.

“SiwezI tena kuchora tattoo kwaajili ya mapenzi. Nimeamua kama tutapendana tutapenda rohoni kwa sababu nishaona hakuna sababu ya kuchora tattoo. Unaweza ukajitolea ukachora tattoo ukazuia mambo yako mengi yanayopita. Nimeona mwenyewe madhara yake kwahiyo mimi
simshauri mtu kuchora tattoo kwa ajili ya mapenzi,” aliongeza.

Hata hivyo Shilole hakuweka wazi sababu ya kuachana na Nuh Mziwanda.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364