-->

Sitozikwa na Wasanii Pekee- Wastara

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amesema hatokuja kumladhimisha mtu yeyote katika tasnia ya ‘bongo movie’ kuwa yeye hana pesa ya kujitibia ugonjwa wake unaomsumbua kwa madai hata siku ikitokea akifa hawezi kuzikwa na hao pekee yao.

Wastara ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha ‘FRIDAY NIGHT LIVE’ (FNL) kinachorushwa na EATV tinga namba moja kwa vijana, baaada ya kuwepo kwa baadhi ya watu kutomuamini kwa kile kinachomsumbua huku wengine wakidiriki hata kujaribu kumwambia anatafuta kiki kupitia tatizo hilo linalomsumbua la mguu wake.

“Yani hapa mtu anaweza akaniumiza kwa maneno au vitendo kwa sababu yeye anaamini kwa mawazo yake na kichwa chake kwamba, mimi nimekaa kitandani siumwi au pengine nimejiona nimepotea katika ulimwengu hivyo natafuta kiki yaani nijifunue nguo niupige picha mguu wangu uliyochanika kisha niuweke kwenye gazeti ama kwenye runinga (Tv) ?”, alihoji Wastara.

Hata hivyo Wastara amesema hawezi kubadilisha fikra za watu wanavyofikilia kwa kuwa hayo ndiyo maisha yao ya kutoamini jambo lolote lile.

“Na kama kuna wasanii ambao wanaamini mimi siumwi siwezi kumladhimisha hata siku moja na ambaye atasema hatokuja kumtembelea Wastara kwa sababu haumwi au hana shida pesa, mimi siwezi kumfanya aniamini kwamba sina pesa. Sitoweza kufanya hicho kitu kwa sababu maelezo ninayoyaeleza katika runinga ndiyo yaleyale hayotokuja kubadilika. Kwa hiyo ninachoongea hapa ni ukweli hautokuja kubadilika miaka yote hata nikifa”, alisisitiza Wastara.

Pamoja na hayo Wastara aliendelea kwa kusema “wapo watu wa kweli wanaoamini na wengine wasioamini ambao huwezi kuwafanya waniamini. Watanzania wanaoniamini mimi wanatosha kwa sababu mwisho wa siku sitokuja kujizika mwenyewe au kuzikwa na wasanii pekee yake”, alisema Wastara.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364