-->

Siwema: Nay Hajanikatisha Tamaa ya Kuwa na Staa

Mrembo aliyezaa na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa, kuingia doa kwa penzi lake na jamaa huyo hakujamkatisha tamaa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye ni staa.

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake,  Siwema Edson

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake, Siwema Edson

Siwema ameliambia Wikienda kuwa hawezi kuapa kwamba hatakaa atumbukie tena kwenye penzi la msanii kwa kuwa hakuna anayejua huko mbeleni ataangukia kwa nani.

“Siwezi kusema kuwa Nay amenikatisha tamaa au sitaingia tena kwenye penzi la staa kwa sababu naweza kuapa halafu ikawa sivyo,” alisema Siwema.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364