-->

Siwezi kugombana na Chege – Juma Nature

Msanii mkongwe nchini Tanzania, Juma Nature maarufu kama ‘Kiroboto’ amefunguka na kusema hajawahi kugombana na msanii mwenzake Chege Chigunda kama watu wanavyofikiri kuwa mwanamke ndiyo amewafanya washindwe hata kusalimiana wawili hao.

Juma Nature (kushoto) na Chege (kulia)

Nature amebainisha hayo baada ya kuenea tetesi za kipindi kirefu zilikuwa zinawaaminisha watu kuwa mke aliyemuoa msanii huyo ndiye alikuwa mpenzi wa Chege hapo awali mpaka kupelekea kuimba wimbo wenye maudhui ya kumuaga mpenzi huyo uliyopewa jina la ‘Good bye’.

“Mimi sijawahi kugombana na mwanangu, sasa mimi nigombane na damu itawezekana kweli ?, hatuwezi kugombana, tutagombana stejini tu kwa sababu ya usanii lakini hatugombani kama hivyo unavyochukulia wewe”. Alisema Juma Nature pindi alipokuwa anazungumza katika kipindi cha eNewz ya EATV

Kwa upande mwingine msanii huyo amesema kwa sasa ameachana na mke wake kwa takribani miaka 7 huku akisisitiza kuwa bado wanaelewana vizuri na hawana ugomvi wowote japokuwa hawapo pamoja tena.

Mtazame hapa kwenye show ya eNewz

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364