-->

VIDEO: Steve Nyerere Afungukia Kutounga Mkono Maandamano ya Bongo Movie

KUFUATIA maandamano ya wasanii wa Filamu nchini, Bongo Movie, ambao wameandamana leo katika mtaa wa Aggrey Kariakoo  wakipinga uingizwaji wa filamu za nje na urudufishwaji wa filamu za ndani huku wakiwataka wamachinga wanaouza filamu hizo waache mara moja, msanii wa tasnia hiyo Steve Mengele Nyerere amefunguka kuhusu kutoonekana kwenye tukio hilo.

Akifanya mazungumzo Global TV Online, Steve ameeleza kuwa sababu ya yeye kutoungana na wasanii wenzake kuandamana ni kwa kuwa jambo hilo halioni kama lina tija kwake.

“Binafsi ninalipinga hili, wasanii tunataka kutumika ndivyo sivyo, siwezi tu kuambiwa kuwa kuna maandamano nikaenda.

“Tunavyosema filamu za nje zinazuia soko la ndani ni uongo, hizi filamu za nje tangu tunazaliwa zilikuwepo, tumewakuta akina Arnold Schweziniger na Rambo, filamu zao zilikuwa zinauzwa Kariakoo. Tulichukua majority yao tukatengeneza filamu zetu. Tuliwakuta Nigeria tukashindana nao tuaweza, hata za filamu za Kihindi tuliweza kushindana nazo.

“Hatujawahi kumzuia Yemi Alade afanye muziki hapa nchini ijapokuwa tuna wanamuziki wetu akina Diamond na Ali Kiba.

“Nachoweza kusema ni kwamba turudi tuangalie ni wapi tumeharibu, tuache kuingiza visingizio ambavyo havina mantiki. Wafanyabiashara Kariakoo wanauza filamu zinazouza na siyo uzalendo.

“Watanzania tumezoea kukaa mezzani na siyo maandamano. Utazuia Dar, je vipi kuhusu Arusha, Dodoma, Mwanza nk… hili janga sio la Dar es Salaam pekee ni la Tanzania nzima.

“Mpaka sasa msambazaji ni mmoja, kaelemewa mzigo, serikali iruhusu wasamazaji wengine waingine kwenye biashara hii.”

“Tumeshindwa kutengeneza radha ya Watanzania, tusiwaadhibu wafanyabiashara, tujiadhibu sisi wenyewe kwa kutengeneza filamu zisizouza.” Alisema Steve Nyerere.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364