Skaina: Sitaki Kuolewa Tena
STAA wa filamu Bongo, Skyner Ally ‘Skaina’ amefunguka kuwa hahitaji kuolewa tena wala kusikia kitu kinachoitwa ndoa katika maisha yake na kwamba anachoshukuru ni Mungu kumjalia mtoto.
Akizungumza na Amani Skaina alisema kuwa, alipata kovu kubwa sana la ndoa kipindi cha nyuma alipofunga ndoa yake ya kwanza hivyo hapendi kusikia tena kitu hicho kwa kuwa tayari amejaliwa mtoto hilo ndilo muhimu kwake.
“Sitaki kabisa kusikia kitu kinaitwa ndoa, naichukia kwanza bora nimeshajizalia mtoto wangu mmoja inatosha,” alisema Skaina.
Skaina alifunga ndoa mwaka 2011 na kijana anayeitwa Saad Omar, ambapo ndoa hiyo ilivunjika baada ya siku nne wakiwa mapumzikoni ‘Honeymoon’ huku kisa kikiwa mwanaume kugundua kuwa msanii huyo alikuwa na ujauzito wa miezi mitano ambao haukuwa wake.