-->

Snura, Ngassa Mnazuga?

WAHENGA wanasema, lisemwalo lipo na kama halipo basi laja. Si mnakumbuka kipindi fulani hivi, staa wa filamu na muziki wa mduara, Snura Mushi na winga nyota wa zamani wa Yanga aliyepo Mbeya City, Mrisho Ngassa picha zao za kiutu uzima ziliwahi kuvuja na kuvumishwa kuwa ni mtu na mtuwe?


Hata hivyo jamaa hao walituzuga hakuna kinachoendelea licha ya picha zile kuwaonyesha wapo kitandani, Ngassa akiwa kalala na kuweka kidole mdomoni mwa Snura aliyekuwa amemwinamia.

Hata hivyo, imefichuka kuwa wawili hao kitambo tu wanakula bata kwa raha zao.

Washakunaku wanadai penzi la wawili hao wala sio siri tena, lakini wenyewe wanashangaa uzushi huo na kudai wanaodai taarifa hizo hawawajui kwa sababu kila mmoja ana mpenzi wake.

“Wewee mimi siwezi kuwa na uhusiano na Ngassa bana, hayo maneno tu, watu wangejua wasingesema ila kiukweli hakuna kinachoendelea na Ngassa, yule ni kama kaka yangu na mtu wangu wa karibu,” Snura alijitetea kwa dhati.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364