-->

Matatizo Yamenifikisha Hapa-Wema Sepetu

Malkia wa filamu bongo, Wema Abraham Sepetu amefunguka na kudai hawezi kubweteka chini na kushindwa kufanya kazi zingine kwa sababu ana kesi mahakamani huku akiamini kwamba matatizo wameumbiwa wanadamu na Mungu ndiye anayepanga.

Wema Abraham Sepetu akiwa na mama yake, siku ya uzinduzi wa filamu yake

Akizungumza na wanahabari kwenye zulia jekundu wakati wa uzinduzi wa filamu yake mpya ‘Heaven Sent’ Mlimani City Century Cinema, Wema amesema matatizo hayapaswi kuchukulia kama sehemu ya kubweteka na kushindwa kufanya mambo ya msingi na kama matatizo yanatakiwa kulelewa basi asingekula asubiri hadi kesi ikiisha ndipo afanye kazi.

“Matatizo tumeumbiwa wanadamu. Siwezi kukaa nikiwaza matatizo yangu kwani Mwenyezi Mungu ndiye anayepanga. Kitu ambacho hakikuui huwa kinakufanya uwe ‘stronger’ hivyo nilitaka kuwaua na mafanikio yangu. Ndiyo nina kesi mahakamani lakini natakiwa kuonyesha watu kwamba wao wanasema hivi lakini ukweli uko hivi. Niseme matatizo niliyopitia ni makubwa lakini yamenifanya niwe hapa. Maisha yamebadilika sana wanasema hapa kazi tu hivyo natumia nafasi niliyonayo ili chakula kiweze kuja mezani na maisha yaeendelee,” Wema.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa filamu yake Wema amesema kwamba kupitia mtandao wake wa ‘Wema App’ ndipo atafanyia mauzo hayo kwani anaamini ulimwengu sasa upo kiganjani.

“Soko la filamu limeshuka hivyo na sisi wasanii inabidi tutumie ujanja wetu ili tuweze kuishi. Ukweli  hali ni ngumu hatuwezi kuficha na imebana sana kwa hiyo movie hii itaanzia kwenye ‘App’ yangu na itapatikana kwa 1500 bei ambayo ni rahisi na kila mtu anayependa kazi za kiafrika naamini haitamshinda kulipia lakini kwa wale watu wetu wa CD watasubiri baada ya muda pia tutatoa kwani hatujawasahau” aliongeza

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364