-->

Snura: Sitaki Mtoto Mwingine wa Nje ya Ndoa

LICHA ya kuwa na watoto wawili kwa baba tofauti, mkali wa kuimba na kunengua, Snura Mushi, amesema kwa sasa hataki apate mtoto mwingine hadi atakapoolewa.

snura567

Msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Chura’ alisema wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi hawakuwa na msimamo na mwelekeo anaoutaka hivyo kwa sasa anataka mwanaume mwenye maadili, imani na upendo kwake, kazi yake na familia kwa ujumla.

“Mimi ni mwanamke, nina watoto wawili kwa sasa na ninatamba na wimbo wangu mpya wa ‘Chura’, lazima nitamani kuolewa lakini sitamani kuwa na mtoto mwingine nje ya ndoa, nataka niolewe na mwanaume mwenyewe awe na imani, mapenzi kwangu na kazi yangu kwa ujumla,” aliesema Snura.

Snura aliongeza kwamba anaamini mwanaume akiwa na imani atapenda muziki wake ambayo ndiyo kazi yake, atampenda yeye na familia yake lakini akikosa imani pia hatokuwa na imani naye.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364