-->

Snura: Sitaki Wanangu Wanifuate

STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi amefunguka kuwa licha ya uanamuziki wake, kamwe hawezi kuwaruhusu wanawe wawe wanamuziki kwani havutiwi na changamoto zilizomo.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Snura ambaye ana watoto wawili, alisema matarajio yake ni kuona watoto wake wakitafuta kazi nyingine kwani wakiwa fani tofauti watakuwa msaada mkubwa kwake.

“Nafanya muziki kwa kuwa natafuta fedha, maisha yamenifanya niingie kwenye fani hii lakini siyo kwamba ndiyo naipenda mpaka niwarithishe na wanangu, sitaki kabisa wawe kama mimi, ukiniuliza kwa nini jibu langu ni hilo, sina sababu, ieleweke hivyo tu, nashukuru Mungu wanangu nao hawana muda na fani hii na ninapenda waendelee kuwa hivyo,” alisema Snura.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364