Jay Dee Ataja Kinachomfanya Aendelee Kuwa Bora
Mwanamuziki Lady Jay Dee kutoka Tanzania amesema kitendo cha yeye kuto-lewa sifa ndiyo kimemfanya kuendelea ku-hit katika soko la muziki ndani na nje ya nchi mpaka sasa.
Msanii huyo amedai kuwa hiyo ndiyo siri pekee iliyomfanya aweze kupita katika vipindi vyote vigumu mpaka leo hii bado yupo katika soko na kuendelea kufanya vizuri kila leo akiachia kazi yake mpya kwa kuwa sifa anazopewa kutoka kwa watu mbalimbali hazimlevyi.
“Ukifanya ngoma na watu wakakujua utakuwa staa lakini usilewe sifa ukilewa mapema utalala alafu utashindwa kuamka…ni miaka kumi na saba sasa, sijawahi kulewa na kila siku naona kama nahitaji kujifunza kitu kipya” Alisema Jay Dee.
Aidha msanii huyo alisisitiza kwa kusema kuwa amekuwepo kwenye muziki takribani miaka 17 bila ya kushuka katika muziki kwa sababu ya kuto-lewa sifa na kufanya vitu vya tofauti kila siku.
Kwa upande mwingine Jide amesema Machi 31 anatarajia kuzindua albamu yake mpya ambayo itakuwa ya saba tangu aanze kufanya muziki.
eatv.tv