-->

Soko la Gigy Money Lipo Huku Kwasasa

Video Queen Gigy Money amesema kwa sasa wasanii wachanga wanamgombania kutaka atokelezee kwenye video zao.

gigy-money18

Gigy Money

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Gigy Money amedai wasanii hao wanaamini akitokelezea kwenye video zao na wao watakuwa wametoboa.

“Kusema kweli sasa hivi underground wananisumbua sana,” alisema Gigy Money. “Wengi wanaamini nikishiriki kwenye video zao ‘nitawakikisha’ na watatoboa. Lakini nashukuru yote ya yote ni biashara wakija ni milioni moja nashiriki kwenye kwenye video kwa sababu ni wengi na bado kwa bei hiyo kuna baadhi wao nawachinjia baharini kwa sababu siwezi kutokea kwenye kila video,”

Pia Gigy alidai kwa sasa yeye ndiye video queen ambaye anafanya kazi nyingi za kulipwa nchini.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364