Christian Bella:Sipendi Kufanya Kolabo
Mkali wa masauti Christian Bella amefunguka kwa kusema kuwa hapendi kufanya sana kolabo kwani zinamfanya azoeleke zaidi na mashabiki wake.
Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa sasa hivi atakuwa anafanya kolabo chache ambazo zitakuwa na faida kubwa katika muziki wake.
“Mimi sipendi sana kufanya fanya kolabo kwa sababu lazima nimlinde Christian Bella,” alisema Bella. “Siwezi kuwa kila muda naimba, huku naimba kule naimba. Lakini mtu akitokea tunafanya na nikiangalia kweli hapa pana umuhimu wa kukaa mimi,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo wake ‘Nishike’ wiki hii amezindua studio yake mpya iitwayo Kingdom Music.