Stanbakora Afunguka Kuoa Mwarabu
MKALI wa vichekesho nchini, Stanley Yusuph ‘Stanbakora’, ameweka wazi kwamba mwakani ndiyo ataoa tena mwanamke mwenye asili ya Kiasia.
Alilifafanulia MTANZANIA kwamba chaguo lake kwa wanawake ni wenye asili hiyo hasa kutoka Uarabuni na awe mcha Mungu.
“Sina mpango na wanawake wa Afrika, napenda mke na mama wa watoto wangu awe mwanamke Mwarabu na anayejua dini,” alisema Stan Bakora.