-->

Stara Atoboa Kinachowapa Umasikini Wasanii

Mwanamuziki mkongwe wa kike nchini Stara Thomas amefunguka na kusema kuwa kuna sababu nyingi sana kwa wasanii wa kike hata wakiume kushuka kimuziki na moja ya sababu kubwa ni kuendekeza sana mapenzi.

Stara Thomas alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai wasanii wengi wanashindwa kurudi kwenye biashara ya muziki kutokana na kukata kwa mitaji ya kuweza kufanya biashara hiyo kutokana na vitendo vyao kama ulevi pamoja na kuendekeza mapenzi.

“Kuna vitu vingi vinavyopelekea mtu kushuka kimuziki kwanza ni ‘mind set’ ya mtu mwenyewe lakini unajua mwanamke kama mwanamke ikifika mahali akiendekeza sana mapenzi lazima ashuke, vilevi wanakula wengine unga, wanakunywa pombe sanaa kwa hiyo wanashindwa kuangalia biashara yao hiyo maana muziki sasa ni biashara, mara anakuja kushtukia msingi wake wa biashara hiyo umekata” alisema Stara Thomas.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364